Mwanamke aliyenyofoa mumewe sehemu za siri kufika mahakamani

Mwanamke mmoja anayekabiliwa na madai ya kunyofoa sehemu nyeti za mumewe na kumsababishia kifo anatarajiwa kufikishwa mahakamani  hapa Mombasa leo Jumatatu kushtakiwa kwa kosa la mauwaji.

Pauline Mukiri mwenye umri wa miaka 32 alitiwa nguvuni na maafisa wa polisi katika eneo la Kiembeni, Bamburi siku ya Jumamosi akijaribu kutoroka.

Kulingana na OCPD wa Kisauni Richard Nagatia mwanamke huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi cha Bamburi anakoendelea  kuhojiwa  kuhusiana na kisa hicho.

Alloys Matata mwenye umri wa miaka 36 mumewe mshukiwa alifariki alipokuwa aktibiwa katika kituo cha matibabu cha Yeshua huko Bamburi.

Kulingana na majirani,mwanamke huyo mwenye ujauzito wa miezi sita alizuru bar moja ambako mumewe alikua akipata kinyuaji na kuanzisha ugomvi akidai hakuwa amewahi kuonekana nyumbani kwao kwa siku tatu zilizopita.

Mwili wa marehemu unahifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya eneo la pwani Coast General.

Total Views: 634 ,