Mwanamke AJikata Mikono ili Alipwe Fidia

Mwanamke mmoja kutoka Slovenia  alichukua msumeno na kukata mkono wake hadi ukakatika kabisa na kuanguka chini ili kampuni ya bima iweze kumlipa fidia na kuwa tajiri wa  Yuro laki nne sawa na shilingi milioni 45.

Familia yake ilimsaidia kwa kuuacha mkono alioukata nyumbani na kumkimbiza hospitali ili hali aisweze kupata matibabu mwafaka na kubakia mlemavu.

Hata hivyo madaktari waligundua hila hiyo na kuutafuta mkono huo na akashonwa na hali yake ikarudi sawa.

Hatimaye njama yake ya kutaka kudanganya kuwa alijikata kwa bahati mbaya alipokuwa anakata miti ikaishia hapo baada ya uchunguzi wa maafisa wa polisi kukamilika, hivyo basi kampuni tano za bima alizokuwa amezichukua zikadinda kumlipa.

 

Total Views: 43 ,