Mwanamke Ajiamini Kusafirisha Wanyama

Kuna watu wamejiamini kutimiza nia zao liwe liwalo.  Mwanamke mmoja kutoka Tawaine amepatikana akiwasafirisha wanyama familia ya  panya 24 huku akiwa amewafunga kwenye miguu yake na kisha kuvaa siruali ndefu. Anasema alifanya ulanguzi huo ili kupelkeka marafiki zake.

Bado ni kitandawili jinsi Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 60  alivyofanikiwa kupita kiwanja ndege huko Uchina alichotumia kusafiri kurudi nyumbani ikizingatiwa kuwa wasafiri hukaguliwa kwa sababu za kiusalama.

Bibi huyo  alisimamishwa na maafisa wa forodha nchini Taiwane  baada ya kumgundua akitembea kimajabujabu.

Na baada ya kumkagua walimpata na wanyama hao hali iliyowashangaza wengi kwa ujasiri wake wa kusafirisha wanyama hao . waliokuwa bado hai na kuchangamka baada ya kuachiliwa.

Kwa sasa anakabiliwa  na shtaka la ukiukaji wa  haki za kuzuia na kudhibiti maradhi dhidi ya wanyama.

Total Views: 113 ,