Mwanamke Adinda Kuenda Kazini Jumapili Mahakama yaagiza Alipwe

Mwanamke mmoja aliyekuwa anaosha vyungu katika hoteli moja huko Miami Marekani amepewa dola milioni 21 sawa na shilingi bilioni 2.1  za Kenya kutokana na nia ya muajiri wake kumulazimisha kufanya kazi jumapili sita 

Marie Jean Pierre alitimuliwa kazi mwaka 2016 kwa kudinda kuenda kazini na badala yake kuenda kanisani.

Mama huyo wa miaka 60 alikuwa amefanya kazi kwa zaidi ya miaka kumi hotelini humo na aliyekuwa anaruhusiwa kuenda kanisani wakati huo hakuona sababu ya kuanza kufungiwa kwenda kanisani ndiposa akaamua kumpeleka muajiri wake mahakamani.

Pia mahakama iliamuru  alipwe shilingi milioni 35 za Kenya alizopoteza kama mshahara wake, shilingi milioni 50 za Kenya za uharibifu wa kumkera kimawazo.

Muajiri wake amesalia kinywa wazi na asema ni sharti akate rufaa.

Total Views: 112 ,