Mwanamke Adai Mumewe Aliuza Figo Yake.

Mwanamke mmoja nchini India anadai kuwa mumewe na kakake wa kambo walipanga njama na kumuibia figo.

Duru zinaarifu kuwa wawili hao wanadaiwa kufanikisha njama yao ili mumewe ajilipe mahari baada ya kumpelekea katika hospitali moja ili kufanyiwa upusuaji alipokuwa na maumivu ya tumbo.

Baadaye mwaka jana , Rita Sarkar alifanyiwa vipimo viwili vya ukaguzi wa kiafya vilivyobaini kwamba alikuwa na figo moja tu.

Anadai kwamba mumewe mara kwa mara alitaka kulipwa mahari yake na kusema kuwa mgogoro huo  wa mahari umemwandama  kwa miaka mingi.

Malipo ya mahari hiyo ambayo hulipwa familia ya mume kutoka kwa familia ya mke nchini India yamepigwa marufuku nchini India tangu 1961.

Total Views: 320 ,