Mvulana wa Miaka 6, apatikana na Kijusi

Madaktari huko India, bado wanatafuta jibu baada ya kufanyia mvulana mwenye umri wa miaka sita upusuaji na kumpta an kijusi tumboni.

Ritesh, alikuwa amelalamikia maumivu ya tumbo kwa miezi mitatu, na madaktari watano waliomfanyia upusuaji kutoa uvimbe, walipigwa na butwaa walipopata ni kichanga kilichokuwa kimeanza kumea mikono, miguu na hata nywele.

Daktari wa watoto  Pradesh asema kuwa kijusi hicho kimekuwepo tangu kijana huyo alipozaliwa .

Ameambia gazeti la Hindustan Times nchini INDIA Kuwa kisa hicho ni miongoni mwa visa vya ajabu na vya  kipekee vitanvyotokea nchini humo.

Hata hivyo mvulana  huyo anaendelea kupata nafuu baada ya kufanyiwa upasuaji huo.

 

Total Views: 650 ,