Mutunga katika Mahakama ya Mombasa

Aliyekuwa jaji mkuu Willy Mutunga alifika mbele ya mahakama  kuu ya Mombasa kama shahidi kwenye kesi ambapo shirika moja lisilo la kiserikali limeishtaki serikali kwa kuliharibia jina. 

Mutunga amefika mbele ya mahakama hiyo kama shahidi wa shirika la Muhuri,ambalo alilianzilisha kwa ushirikiano na marehemu Profesa Alamin Mazrui mwaka 1997.

Shirika hilo limewashtaki mwanasheria mkuu,inspekta jenerali wa polisi,benki kuu ya Kenya kwa uharibifu lilipohusishwa na kundi la kigaidi la Al-shabaab mwaka 2015.

Total Views: 174 ,