Mutunga alitaka bunge la Seneti kuwajibikia Ugatuzi

Jaji mkuu Dkt Willy Mutunga amelitaka Bunge la Seneti kuulinda ugatuzi vilivyo iwapo kenya ni inufaike kutokana na utajiri wake wa rasilimali.

Mutunga aliyepewa fursa ambayo ni nadra zaidi kulihutubia bunge la seneti amesema kuwa bunge hilo jipya chini ya katiba mpya halistahili kufinyiliwa ila lijitokeze na kutekeleza wajibu wake vilivyo kwa mujibu wa katiba.

Jaji Mutunga anaingia katika historia ya taifa hili kama jaji wa kwanza aliye mamlakani kuwahi kulihutubia bunge la Seneti ambapo ametoa wito kwa mabunge mawili nchini kujiepusha na mvutano wa ni lipi lililo na mamlaka kuliko lengine.

Mwisho

Total Views: 401 ,