Mudavadi amtaka rais kuharakisha idhinisho la kujiuzulu kwa baadhi ya makamishna wa IEBC

Kiongozi wa muungano wa Amani National Congress Musalia Mudavadi amepongeza hatua ya makamishina wa tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kutaka kujiuzulu na kumhimiza rais Uhuru Kenyatta kuharakisha hatua hiyo ili kuharakisha utatuzi wa mizozo kwenye tume hiyo.

Kwenye taarifa kwa vyombo vya habari Mudavadi amesema makamishna watano waliobaki wanapaswa kuchukua mkondo sawia wa wenzao wanne ambao tayari wameashiria kujiuzulu ili kuipunguzia mzigo kamati inayoshughulikia mzozo huo wa IEBC.

Kadhalika ameeleza kuwa hatua hii pia ni njia moja wapo ya kufanikisha matayarisho kabambe hasa wakati huu taifa linapojiandaa kwenye uchaguzi mkuu ujao.

Miongoni mwa makamishina walioandika barua kwa rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne kutaka kujiuzulu ni pamoja na Yusuf Nzibo, Albert Bwire, Kule Galma na Abdullahi Sharawe.

Mwisho

Total Views: 341 ,