Mtoto maajabu………………

Katika Malimwengu na Walimwengu…………….

Msichana wa umri wa miezi sita amevunja rekodi kwa kuwa mtu wa umri mdogo zaidi duniani kuwahi kushiriki mchezo wa kuteleza majini.

Zyla St Onge aliteleza umbali wa mita-209 akiwa pekee yake kwenye ziwa moja katika jimbo la Florida nchini Marekani huku wazazi wake wakiogelea kando yake.

Hata ingawa hajaweza kutembea, mtoto huyo alijizatiti na kuteleza kwa ustadi mkubwa.

Wazazi wa mtoto huyo wanadai kuwa huyo ni mtoto wakipekee kwani huwasiliana na Mungu moja kwa moja na kisha kuwapa ujumbe kwa njia ya ishara licha ya kuwa hajaweza kufikia umri wa kuweza kuongea.

Mwisho

Total Views: 577 ,