Msuko suko Sudan Kusini,mataifa yawahamisha raia wake

Nchi kadha zimeanzisha mikakati ya kuwaondoa raia wake kutoka nchini Sudan Kusini kufuatia siku kadha za machafuko yaliyosababisha kuuwawa kwa mamia ya watu nchini humo.

Ujerumani,Uingereza,Italia,Japan,India na Uganda ni miongoni mwa mataifa yaliyoanza mikakati ya kuwaondoa raia wake kutoka nchi hiyo ili kuhakikisha kuwa wanakuwa salama kutokana na vurugu hizo.

Tayari msafara wa kijeshi kutoka uganda ulio na takriban magari hamsini ambayo baadhi ni ya kivita ulivuka mpaka katika eneo la Nimule kilomita mia mbili kutoka Juba ili kuwanasua raia wake takriban elfu tatu wanaotaka kutoroka mapigano hayo.

Mwisho

Total Views: 607 ,