mshirikishi wa eneo la Pwani amkashifu gavana joho kwa kuendeleza ukatili dhidi ya wapinzani


Mshirikishi wa eneo la Pwani Nelson Marwa amemkashifu gavana wa Mombasa Hassan Joho kwa kuwazuiya wapinzani wake kuweka mabango yao ya kampeni katika eneo hili.

Akiwahutubia waandishi baada ya kufanya ziara ya gafla katika kivukio cha Mtongwe,Marwa pia  amewakashifu askari kwa kumkinga mwanasiasa huyo kuendeleza ukatili akisema ni haki ya kila mwanasiasa kuweka bango.

Hatua ya Marwa inajiri baada ya wawaniaji wa ugavana katika kaunti hii ya Mombasa kupinga agizo linalosemekana kutolewa na Joho la kuwazuiya kuweka mabango yao ya kampeni za uchaguzi mkuu.

Wagombea hao wanaojumuisha Suleiman Shahbal  wa Jubilee, Hassan Omar wa Wiper na Hezron Awiti  wa chama Vibrant Democratic wamedai watu wanaohusika na matangazo ya kibiashara wamepewa maagizo ya kutowaruhusu kuweka mabango yao.

Total Views: 291 ,