MSAKO WA WANAFUNZI KAUNTI YA KWALE

Msako dhidi ya wanafunzi ambao hawajajiunga na shule za upili umeanza rasmi kaunti ya Kwale huku wadi ya Kinondo ikiwa ya kwanza kutekeleza agizo hilo.

Akizungumza na wanahabari katika eneo la Nyumba Mbovu huko Kinondo kaunti ya Kwale wakati wa kuzindua kampeni hiyo,chifu wa eneo hilo Ali Riga amesema kuwa wamefanikiwa kuwapata wanafunzi 92 kati ya 98 wanaofaa kujiunga na shule ya upili.

Chifu huyo amedokeza kuwa wananuia kuwasajili wanafunzi hao katika shule zilizo katika eneo hilo huku huku kampeini ya kuwasaka wanafunzi wengine ikiendelea.

 

Total Views: 72 ,