Msako dhidi ya wanasiasa wa Upinzani kuendelea asema Boinnet

Inspekta jenerali wa polisi Joseph Boinnet anasema msako dhidi ya wanasiasa wa upinzani utaendelea licha ya shtuma na malalamishi.

Akiongea katika cha mafunzo kwa maafisa wa polisi cha Kiganjo, Boinnet amekanusha ukiukaji wa sheria na haki za kikatiba za wanasiasa ambao wamekamatwa  kwenye msako ulioanza baada ya hafla tata ya kuapishwa kwa kiongozi wa upinzani Raila Odinga.

Aidha amewatahadharisha wanasiasa kwamba hawatasazwa katika juhudi za kudumisha sheria na utangamano hapa nchini.

Alisema haya wakati wa siku ya kwanza ya kujifahamisha na huduma ya taifa ya polisi, akisema hafla nyingine sawa na hiyo zitaandaliwa katika chuo cha mafunzo kwa polisi wa utawala cha Embakasi na kile cha mafunzo kwa maafisa wa kitengo cha GSU.

Mwisho

Total Views: 200 ,