MSAKO DHIDI YA TAASISI BANDIA ZA UANAHABARI

Afisa mkuu katika baraza la kitaifa la uanahabari David Omwoyo ameeleza kuwa hivi karibuni wataanza msako wa kubaini taasisi ambazo hazina vibali vya kutoa mafunzo kuhusu taaluma ya uanahabari na kuzifunga.

Akizungumza baada ya kufanya mkutano wa kutoa hamasa kwa wanahabari hapa Mombasa Omwoyo amesema kuwa taasisi mbalimbali hapa Mombasa, Nairobi, Eldoret, Kisumu na Kakamega baadhi yazo ndizo zimeripotiwa kutoa mafunzo hayo bila kibali.

Ameeleza kuwa baada ya tangazo watakalochapisha katika magazeti ya humu nchini mwishoni mwa mwezi huu ndipo wataanza msako huu.

Hatua hii inajiri kufuatia utafiti uliofanywa na baraza hilo kwamba kuna baadhi ya wanahabari nchini bandia huku wengine wakiwa wamepata stakabadhi zao kutoka kwa taasisi zisizotambulika.

Picha hisani.

Total Views: 24 ,