MPISHI AJITIA KITANZI HUKO KAMBE KILIFI

Mwanamume ambaye alikuwa mpishi  katika shule ya upili ya Kambe kaunti ya Kilifi amejitia kitanzi mapema leo.

Kulingana na chifu wa eneo hilo Carlson Matsaki Mtsonga,marehemu alipatikana akining’inia kwenye  nyumba ya kuhifadhia kuni ya shule hiyo.

Mwenda zake kwa jina Dickson Ruwa Makonde,mkaazi wa Kambe Mbungoni anasemekana aghalabu hurauka kuwaandalia wanafunzi na walimu kiamshwa kinywa.

Haijabainika sababu zilizomfanya kujitoa uhai ingawa inashukiwa huenda hatua hiyo ilisababishwa na matatizo ya kinyumbani.

Polisi wameanzisha uchunguzi kubaini sababu halisi zilizomfanya mwanamume kujiuwa

Total Views: 35 ,