MOTO WATEKETEZA MALI LEOPARD BEACH DIANI

Mali ya mamilioni ya pesa imeteketea baada ya moto kuzuka katika hoteli moja huko Diani kaunti ya Kwale jana usiku.

Kulingana na afisaa mkuu wa polisi kaunti hiyo Tom Odero,moto huo ulizuka mwendo wa saa nne  katika hoteli ya Leopard Beach na kusambaa hadi maeneo jirani.

Hata hivyo kamanda huyo wa polisi amesema kuwa hakuna hata mtu mmoja aliyejeruhiwa kwenye kisa hicho.

Odera anasema wageni waliokuwa kwenye hoteli hiyo walihamishwa haraka hadi maeneo salama huku baadhi ya mali pia ikihamishwa

Afisaa huyo wa polisi amesema chanzo halisi cha mkasa huo hakijabainika lakini uchunguzi unaendelea.

Hata hivyo baadhi ya wahudumu wa magari ya kitalii waliokuwa karibu na hoteli hiyo wakati wa mkasa huo wanadai ulipuaji wa fataki ndio uliosababisha moto huo.

Inasemekana kuwa onyo lilikuwa limetolewa siku za nyuma dhidi ya ulipuaji wa fataki katika eneo hilo.

Total Views: 83 ,