Mmliki na Msimamizi wa Bwawa la Patel Wajisalimisha

Mmliki wa bwawa la Patel Mansukh Kansagara na msimamizi mkuu Vionj Kumar wamejisalimisha kwenye kituo cha polisi cha Naivasha siku moja baada ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma kuagiza wakamatwe na kushtakiwa.

Noordin Haji anataka wawili hao kushtakiwa pamoja na maafisa wa serikali kuhusiana na mkasa uliopelekea watu 47 kuaga dunia wakati bwawa hilo katika eneo la Solai lilipopasuka na kusababisha hasara katika kijiji jirani.

Wawili hao wanawakilishwa na Evans Monari aliyetoa taarifa jana Jumatano usiku alisema wamekuwa wakishirikiana kikamilifu na mamlaka husika wakati wa uchunguzi.

Total Views: 128 ,