MMILIKI WA MKAHAWA UCHINA ATOA OFA YA KUCHEKESHWA

Mmiliki wa mkahawa mmoja huko Kusuni Magharibi mwa Uchina amezindua ofa  ya aina yake ambapo anawapunguzia wateja watakaomchekesha.

Surnamed Chen anasema wateja watapa ofa kwa viwango tofouti kulingana na  viwango vya vichekesho. Iwapo mteja atamfanya atabasamu basi ataondolewa gharama ya malipo kwa asilimia 10 na iwapo atamfanya acheke zaidi basi atamuondolea kwa asilimia 50.

Jarida la Beijing news linasema mwanamke mmoja alipunguziwa chakuka kwa asilimia 30 baada ya kumuonyesha video ya kuchekesha aliyoipenda tu na wala haikumchekesha.

Jamaa huyo anasema lengo kuu la kufungua mkahawa huo ni kuwa na wakati mwema na wateja wake na kuwa na mwingi wa furaha na si kutengeneza faida.

Total Views: 20 ,