Mlevi Apigia Simu Polisi Akidai Yeye ni Mlanguzi

 

Hebu tafakari haya. Mtu kulewa na kutazama filamu  kwenye runinga na kufikiri kuwa ni maisha yake halisi na kuita maafisa wa polisi waje wamukamate.

Haya ndio yaliyomfikia mwanamume mmoja huko Uchina aliyekuwa amelewa chakari. Mwanamume huyo anasemekana alikuwa anatazama filamu moja iliyosimulia jinsi afisa mmoja wa polisi jasiri alivyofanikiwa kumtia nguvuni mlanguzi sugu  wa dawa za kulevya.

Kisha katika hali yake ya kulewa akifikiri kuwa mlanguzi huyo alikuwa ni yeye  na kuwapigia  maaifisa wa polisi simu mara 17 kuwa ni mlanguzi na hata ameumua mtu dakika chache kabla ya kuzungumza nao.

Maafisa wa polisi walimuonya mara kadhaa kuwa angeadhibiwa kwa kuwadanganya.

Aliendelea kuwarai  maafisa wa poliisi kumkamata na hatimaye wakamakamata kweli na wakimuzuilia kwa siku saba.

Baadaye walipomhoji waligundua kuwa alikuwa akiwadanganya na wakamtoza faini ya yuan 200 sawa na shingi elfu mbili na mianane za Kenya.

Total Views: 24 ,