MKURUGENZI NA WAANGALIZI

Afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imesema kuwa imeweka mikakati ya kukabiliana na makosa ya uchaguzi yanayojumuisha matamshi ya chuki,uchochezi wa ghasia, mateso na uharibifu wa mali.

Akiongea kwenye warsha ya vyombo vya habari kuhusu utayari wa uchaguzi katika kaunti ya Machakos,naibu mkuu mkurugenzi wa mawasiliano ya umma Beatrice Omari amesema afisi ya mkurugenzi wa mashtaka ya umma imewapa mafunzo mahakimu 105 maalum kushughulikia makosa hayo.

Mkurugenzi wa ashtaka ya umma Keriako Tobiko amesema afisi yake itashughulikia makosa ya uchaguzi ambayo yametokea tangu kuanza kwa shuhguli ya usajili wa wapiga kura,wakati wa kura za mchujo na yale yatakayojiri wakati wa uchaguzi mkuu wa tarehe 8 mwezi Agosti.

Omari amedokeza kwamba kufikia sasa watu 62 miongoni mwao wagombea wa ugavana,mbunge na wawakilishi wa wadi walio mamlakani wanakabiliwa na kesi za uchaguzi mahakamani.

Pia ameongeza kuwa afisi hiyo imeanzisha kituo cha kupiga simu cha saa 24 ambapo umma unaweza kuripoti kasoro za uchaguzi na kwamba mkataba wa makubaliano tayari umesainiwa kati ya afisi hiyo na tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC kuhakikisha maafisa wanatoa ushahidi kotini dhidi ya uhalifu unaohusiana na uchaguzi.

Total Views: 304 ,