Mjumbe wa wodi ya Bamba huko Kilifi ainyoshea kidole serikali kuu

 

Mwakilishi wa wadi ya Bamba kaunti ya Kilifi Daniel Mangi ameilaumu serikali kuu kutokana na shida ya uhaba wa maji inayoendelea kuwakumba wakaazi wa eneo bunge la Ganze.

Mangi amesema kutobadilishwa kwa mifereji inayotoka kituo cha kusukuma maji cha Baricho ndio chanzo kikuu cha uhaba huo kwani mifereji hiyo hupasuka kila mara maji yanaposukukumwa

Hata hivyo amesema kuwa serikali ya kaunti ya Kilifi imeshirikiana na shirika la msalaba mwekundu kutekeleza mradi utakao hakikisha shida ya maji katika kaunti ya Kilifi hasa Ganze inatatuliwa kikamilifu.

Zaidi ya shilingi milioni mia moja zimetengwa kusimamia mradi huo ambapo kwa sasa Mangi amesema mikakati ya ununuzi wa vifaa vinavyohitajika unaendelea .

Total Views: 400 ,