Michael Mwandigha

Michael Mwandigha ni mtangazaji mwenye sauti ya kuvutia katika kusoma habari pamoja na kufanya matangazo ya kibiashara. Ni mtu mcheshi sana na ana kipaji cha kuigiza sauti za wanahabari wenzake zaidi ya 9 kutoka vituo mbali mbali vya habari pamoja na wanasiasa. Mwandigha ni mwanaspoti anayeshabikia klabu ya Chelsea. Hupenda sana mlo wa sima na Nyama na kwake kitambi na hamu ya kula ni baraka kutoka kwa Maulana.

Total Views: 988 ,