MGOMO WA WAUGUZI

Wanachama wa muungano wa wauguzi nchini walifanya maandamano leo jijini Nairobi na kuelekea hadi katika afisi za wizara ya afya kuwasilisha lalama zao.

Kaimu katibu mkuu wa KNUN Maurice Opetu amesema tume ya kuwianisha mishahara SCR,Bodi kuu ya huduma katika kaunti na baraza la magavana wamepokea stakabadhi hiyo ya malalamishi.

Ameongeza kuwa kwa sasa wanasubiri matokeo kutoka kwa pande husika huku muungano wa vyama vya wafanyikazi nchini ukipendekeza kushirikishwa kwenye mazungumzo ya utatuzi wa mzozo huo kama mpatanishi.

Afisa kutoka COTU Benson Okwaro amesema majadiliano hayo yataandaliwa kesho jijini Nairobi ambako maafisa wa waizara ya leba na wale wa KNUN wanatarajiwa kushiriki.

Haya yanajiri huku mgomo huo wa wauguzi ukiingia siku yake ya nane tangu ulipoanza huku taasis nyingi za afya nchini zikisalia mahame.

Wauguzi wanaogoma wanataka mwajiri wao asaini na kuusajili katika mahakama ya Leba mkataba wa makubaliano ya pamoja ulioafikiwa mwaka uliopita.

Total Views: 366 ,