Mfalme Abdulla wa pili kutoka Jordan yuko nchini

 

Mfalme Abdulla wa pili Bin Al-Hussein wa Jordan ataanza ziara yake humu nchini leo Jumatatu ambapo anatarajiwa kufanya mkutano na rais Uhuru Kenyatta miongoni mwa shughuli nyingine.

Msemaji wa Ikulu Manoa Esipisu amesema mfalme Abdulla na rais Uhuru Kenyatta wataongoza hafla ya kufungwa kwa warsha kuhusu  usalama na ujuzi wa kukabiliana na changamoto ibuka za usalama katika shule ya Embakasi Garrison.

Warsha hiyo inayofahamika kama Swift Eagle ni warsha ya siku tisa ya mazoezi ya kijeshi yanayolenga kubadilishana ufahamu na ujuzi katika kukabiliana na changamoto ibuka za kiusalama.

Kenya inakumbwa na tishio la kigaidi kutoka kundi la wanamgambo  la Alshabaab kutoka Somalia na  washirika wake Isis hatua inayoonekana ya kulipiza kisasi kupinga vita vilivyoanzishwa na majeshi ya ulinzi ya kenya nchini Somalia mwaka 2011.

Total Views: 339 ,