Mbuzi Achaguliwa kuwa Meya

Wanasema ukistaajabu ya musa utayaona ya firauni, Mbuzi mwenye umri wa miaka 13 anayejulikana kama Lincoln amechaguliwa kuwa meya wa mji wa Fair Haven.

Lincoln atakuwa meya kwa muda wa mwaka mmoja wa mji huo unaopakana na jiji la Newyork  ulio na watu takriban 2,500 na hauna meya binadamu.

Lincoln aliwabagwa wapinzani wake baada ya kupata kura 13, mpinzani wake wa karibu Mbwa anayejulikana kama Sammie akipata kura 10  na wanyama wengine wakapata  kura 30 kwa pamoja.

Uchaguzi huo ulifanyika kwenye mkutano na wanajamii wa mji huo.

Atakuwa na jukumu la kukagua gwaride wakati wa siku za kitaifa huku akiwa amevalia sare rasmi.

Total Views: 105 ,