Mbunge wa Mavoko azuiliwa

Mbunge wa Mavoko Patrick Makau anazuiliwa na maafisa wa polisi baada ya kujisalimisha mwenyewe kwa idara  ya upelelezi  mapema leo.

Mbunge huyo anachunguzwa kufuatia madai ya kuwachochea vijana na waendesha bodaboda kuchoma kituo cha polisi tawala cha Syokimau mwishoni mwa wiki  ambapo inasemekana  wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi walizuiliwa  kabla  kuuawa.

Maafisa wa polisi wanasema uchunguzi unaendelea.

Total Views: 422 ,