MAWASCO NA KIMAWASCO

Pendekezo la kuainisha kampuni mbili za maji katika kaunti ya Kilifi limezua hisia tofauti miongoni mwa wadau na wakaazi  eneo hilo.

Tangazo hilo lilitolewa kwenye mkutano wa  kila mwaka wa kampuni ya usambazaji maji ya MAWASCO   uliofanyika huko Malindi ambao baadhi ya wadau walipinga pendekezo hilo wakisema hatua hiyo itaathiri utoaji wa huduma za maji katika kaunti hiyo.

Mmoja wa maafisa katika kampuni ya Mawasco Philip Chai,anasema hatua ya kuainisha kampuni hizo mbili Mawasco na KIMAWASCO itatatiza huduma za maji katika miji mikubwa kaunti hiyo ikiwemo  Malindi, Kilifi, Mtwapa, Mariakani na Mazeras.

Badala yake Chai anapendekeza kufanywa kwa uchunguzi wa kina kabla ya kufanya uamuzi wa kuwa na kampuni moja ya maji kaunti hiyo.

Picha kwa hisani

Total Views: 83 ,