Maskwota Msambweni Kutabasamu hivi Karibuni

Serikali ya kitaifa inasema itawakabidhi hati miliki za ardhi zaidi ya maskwota elfu tano wanaoishi katika eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale katika kipindi cha  miezi mitatu ijayo.

Akizungumza na  maskwota hao  katika ziara yake kaunti hiyo katibu katika wizara ya ardhi Nicholas Muraguri amesema mikakati inaendelea kuhakikisha kila mmoja anapata hati miliki  ili kupunguza idadi ya maskwota.

Mbunge wa Mswambweni Suleiman Dori aliyekuwa ameambatana na katibu huyo katika ziara hiyo ameishtumu tume ya ardhi nchini kwa kile alichokitaja kuwa vikwazo katika ardhi zenye utata.

Total Views: 144 ,