MASIKITIKO YA MRADI WA GALANA KULALU

Baadhi ya viongozi kutoka kaunti ya Kilifi wameeleza masikitiko yao kufuatia kuendelea kusambaratika kwa mradi Galana Kulalu ulioigarimu serikali mabilioni ya fedha.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari naibu gavana wa kaunti hiyo Gideon Saburi na mbunge wa Ganze Teddy Mwambire sasa wanaishinikiza serikali kuziruhusu serikali za kaunti ya Kilifi na Tana River kuusimamia mradi huo.

Kulingana na viongozi hao japo rais Uhuru Kenyatta alinuia kukabili uhaba wa chakula ambao umekuwa ukiyakumba baadhi ya maeneo nchini kwa kuutumia mradi huo, lengo hilo linaendelea kufifia.

Ikumbukwe Serikali ilitenga shilingi bilioni 7.2 kwenye mradi huo uliolenga upatikanaji  wa chakula humu nchini kupitia unyunyuzia maji kwenye shamba la ekari nusu milioni ambalo mradi huo umekuwa ukitekelezwa.

Picha kwa hisani.

Total Views: 57 ,