Mashindano ya Ngamia Saudia Arabia

Ngamia 12 wameshindwa mashindano ya urembo nchini Saudi Arabia baada ya wamiliki wao kuwadunga sindano ya kubadili maumbile.

Maelfu ya ngamia wameshirikiswa katika tamasha la Mfalme Abdulaziz na kushindana  kwa kuonyesha  nyuso zao, nundu na maumbile yao.

Lakini majaji waliingia kati wakati walipogundua kwamba baadhi ya udanganyifu ulifanyika na baadhi ya wamiliki waliotaka kushinda tuzo za fedha.

Jaji mkuu Fawzan al-Madi amesema kuwa ngamia ni moja wapo wa “nembo ya Saudi Arabi”

Mashindano hayo ya urembo wa ngamia yalifanyika kwa mara ya kwanza mwaka 2000.

Vile vile tamasha hilo lina mashindano ya riadha ya ngamia na kuonja maziwa, lina tuzo ya fedha taslim dola milioni 57.

Total Views: 171 ,