Masharti ya Michezo ya Bahati Nasibu Kujadiliwa na Bunge

Bunge linatarajiwa kujadili mswada ambao ukipitishwa utawezesha kutekelezwa mabadiliko makubwa katika michezo ya bahati nasibu,kubashiri matokeo na uchezaji kamari .Mswada huo uliowasilishwa na mbunge wa Gem Jakoyo Midiwo, unapendekeza kuongezwa kwa ushuru unaotozwa washindi kwenye michezo hiyo, na pia kuweka kiwango cha pesa mtu binafsi anaweza kujishindia.Aidha mswada huo unapendekeza kwamba wanaoshiriki michezo hiyo wawe na umri wa miaka 25 au zaidi.Mswada huo pia unapendekezwa saa kubashiri matokeo ya michzeo kuwa kati ya saa moja asubuhi na saa moja jioni.Ukipitishwa,mswada huo utawazuia raia wa kigeni kumiliki kampuni za uchezaji kamari kwa njia ya mtandao.

Total Views: 389 ,