MASENETA WASIMAMISHA USAJILI WA NIIMS

Kamati ya Usalama katika bunge la seneti imeiagiza wizara ya usalama wa ndani kusimamisha mara moja usajili mpya wa raia unaoendelea kupitia mfumo wa NIIMS,katika vituo vya huduma centre.

Wamachama wa kamati hiyo akiwemo seneta wa Bungoma Moses Wetangula,wanadai kuwa data inayokusanywa huenda ikatumiwa vibaya hivyo basi kuhatarisha maisha ya wakenya.

‘’Ulinzi wa data za watu binafsi ni muhimu sana,huwezi kuanza kukusanya habari muhimu kuwahusu wakenya kama vile DNA bila kufafanua itakavyotumika’’

Kamati hiyo badala yake imewataka waziri wa usalama wa ndani Dkt.Fred Matiang’i, mwenzake wa teknologia,habari na mawasiliano Joe Mucheru na mwanasheria mkuu Paul Kihara,kufika mbele yake mnamo tarehe 11 mwezi Machi  kwa majadiliano zaidi.

Maseneta hao wanasema usajili huo hautaendelea hadi uidhinishwe na viongozi wa kisiasa.

‘’Usajili huo usimamishwe hadi tufanye majadiliano,mkiwa mko tayari hata kesho tutakaa tujadiliane pamoja’’

Usajili huo ambao umekuwa ukiendelea katika vituo vya huduma centre kote nchini ulizinduliwa rasmi na katibu wa wizara ya usalama wa ndani Karanja Kibicho mnamo tarehe 18 mwezi huu.

Total Views: 112 ,