Marufuku dhidi ya Mifuko ya plastiki yatekelezwa

Mamlaka ya usimamizi wa Mazingira nchini NEMA inatekeleza msako kote nchini kuhakikisha kuwa wafanyibiashara wa reja reja na wazalishaji bidhaa wametekeleza marufuku ya matumizi ya mifuko ya Plastiki inayotekelezwa nchini.

Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Geoffrey Wahungu amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo ili kuhakikisha kuwa sheria inatekelezwa vilivyo akieleza kuwa tayari wameweka maafisa wa kushinikiza utekelezaji huo kote nchini.

Amesema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo kwa juma moja kama njia moja wapo ya kutoa hamasa kwa umma huku wakifanya uchunguzi wa jinsi wazalishaji bidhaa,wauzaji wa rejareja na biashara mbali mbali zinavyotekeleza marufuku hiyo.

Mwisho

Total Views: 216 ,