Marcos Alonso kutua Chelsea

Mkufunzi wa klabu ya Chelsea Antonio conte anaelekea kukamilisha usajili wa Marcos Alonso kutokea Fiorentina kwa kima cha euro milioni 23 ili kukamilisha safu yake ya ulinzi.

Difensi ya Chelsea inahitaji ngangari na usajili mwingine utaimarisha safu hiyo inayoongozwa na Cesar Azpillicueta, Gary Cahill, John Terry na Kurt Zouma.

Zouma atasalia kikosini Chelsea licha ya klabu ya Schalke’04 kumtaka kwa mkopo,aidha angali mkekani akiuguza majeraha.
Huku hayo yakijiri Cesc Fabregas amepuzilia mbali nia ya Conte kutaka kumwondosha katika klabu ya Chelsea akisema hakuwa amefahamishwa hilo.

Conte alitaka kumwuza Fabregas kwa klabu ya Real Madrid ila klabu ambayo ndio mabingwa wa bara europa wamekataa huduma zake.
Aidha Conte yupo katika hatua za mwisho kutwaa mchezaji Marcelo Brozovic kutokea klabu ya Intermillan kiungo mwenye umri wa miaka 23 kwa kima cha euro milioni 25.

Marcelo ameichezea Intermillana mara 47 na kufunga mabao 5

Total Views: 570 ,