Maraga:Mahakama na Uchaguzi

Jaji mkuu David Maraga amesema kuwa idara ya mahakama itapeana taarifa kamili kuhusiana na kesi zinazoendelea mahakamani kuhusu matayarisho ya uchaguzi mkuu ujao.

Akizungumza wakati wa hafla ya kuapishwa kwa zaidi ya mawakili 50 Maraga amekataa kuzungumzia iwapo kesi zilizowasilishwa na muungano wa NASA na mashirika ya kijamii mahakamani zinaweza kusababisha kuchelewa kwa uchaguzi.

Amewataka mawakili walioapishwa kuhakikisha kuwa wanapigania utekelezaji wa haki nchini huku akisema kuwa idara ya mahakama nchini imeshuhudia mabadiliko mengi kinyume cha ilivyokuwa awali kabla ya kuwa asasi huru.

Mwisho

Total Views: 224 ,