Mapenzi ya simu, Karaha

Malimwengu na Walimwengu…

Wanasema walimwengu mapenzi ni kikohozi na kamwe hayafichiki…na anapopenda mja bila shaka ikawa mume au mke hupenda pia kumiliki mpenziwe na kila kitu chake..lakini hili nalo lashangaza…

Mwanamke mmoja katika muungano wa milki za kiarabu amepigwa faini na hatimaye kurudishwa kwao baada ya kupatikana na hatia ya kuingia  katika faragha ya mumewe.

Vyombo vya habari nchini humo  vinasema kuwa mwanamke huyo alichukua na kufungua simu ya mumewe baada ya kumshuku kwamba alikuwa na uhusiano wa kando na akaanza kudurusu kharafa,pamoja na picha zilizokuwemo ndani ili kupekua nani anayetaka kugawa penzi lake.

Mumewe alilalamika kwa maafisa wa polisi na mkewe na hatimaye alikamatwa na kushtakiwa  chini ya sheria ya uhalifu wa mtandaoni na  mwanamke huyo ambaye jina lake lilibanwa na ambaye pia ni mgeni katika muungano wa milki za kiarabu alipigwa faini ya pauni 28,000.

Mwanamke huyo aidha alikiri mahakamani  kwamba aliifungua simu ya mumewe bila ya ruhusa na kuzituma picha katika simu yake..maajabu hayo wapenzi hao amabao wote wana miaka 30 waliwacha wengi na mshangao kuhusu mahaba yao…

Ama kweeeli Kisichofanana na mwenyewe, ni cha kuiba….

Mwisho

Total Views: 860 ,