Mapenzi tele na Zumbukuku

Leo ikiwa ni ya  wapendano maarufu Valentine’s Day na wanasema wavyele kipendacho roho hula nyama mbichi.Mwanamke aliyeolewa na zumbukuku maarufu kama Zombie Doll sasa anasema wanampango wa kutafuta watoto.

Felicity Kadlec mwenye umri wa miaka 20 aliyeolewa na Zumbukuku anayedai ana umri wa miaka 37 asema hamna kitakachomtenganisha  na mpenziwe  na kwamba wananuia kupata msamaria mwema ili kuwatolea mbegu za kiume.

Wawili hao wanaishi Oklahoma na wanasema wana makaazi bomba na itakuwa kamili endapo watakuwa na watoto.

Wapenzi hao walifunga ndoa kwenye sherehe ya kufana huko nchini Marekani iliyohudhuriwa na mazumbukuku  wengine wanane marafiki wa bwana harusi.

Total Views: 102 ,