Maoni Kuhusu kuunda Chama cha Pwani.

Kauli ya gavana wa kaunti ya Kilifi Amason Kingi ya wenyeji wa Pwani   kubuni chama chao inaendelea kuzua hisia tofouti

Mbunge wa Kaloleni Gunga Mwinga ameunga mkono  hatua hiyo huku akisisitiza kuwa chama hicho ni shariti kizingatie katiba ya Kenya na sheria ya vyama humu nchini.

Mhadhiri wa chuo kikuu cha Pwani   Prof Halim Shauri   amewataka viongozi kutoka eneo hili la Pwani kukomesha ubinafsi na kuungana ili  kufanikisha lengo la kuunda chama chao huku akisisitiza kuwa hiyo  ndio njia pekee ya kufikia malengo ya wapwani kitaifa.

Total Views: 182 ,