Man united kikaangoni Asema Mou

Mkufunzi wa klabu cha Manchester united Jose Mourinho ametoa tahadhari kwamba huenda klabu hicho kikakabiliwa na “msimu mgumu” iwapo hawataimarisha kikosi chao kwa kuwanunua wachezaji wapya kabla ya kipindi cha uhamisho kufungwa Alhamisi.

Haya yanajiri baada ya Mashetani Wekundu kukamilisha mechi za kirafiki za kujiandaa kwa msimu mpya kwa kuchapwa 1-0 na mabingwa wa Ujerumani Bayern Munich siku ya Jumapili…

Kufikia sasa United wamewanunua wachezaji watatu ambao ni kiungo wa kati Mbrazil Fred aliyewagharimu £47m, beki Mreno Diogo Dalot na kipa nambari tatu Lee Grant.

Aidha wachanganuzi wa soka nchini Uingereza wanamtaka Mourinho kutafuta mbinu ya kumaliza mzozo kati yake na afisa mkuu mtendaji wa klabu hicho Ed Woodward.

Total Views: 171 ,