Mama Anayechimba Madini Taita Atoa Ushauri

Wito umetolewa kwa Vijana na akina mama kaunti ya Taita Taveta kutochagua kazi na badala yake kujishughulisha na uchimbaji madini ili kukakabiliana na ukosefu wa ajira miongoni mwao.

Kulingana na Peris Mramba,mmoja wa wachimba madini katika kaunti hiyo anasisitiza  amekuwa akijitimizia mahitaji yake binafsi bila kutegemea yeyote kwa uchimbaji madini hivyo kuwataka akina mama wenzake kumuiga na kuacha  kutegemea waume zao  kwa mahitaji yote.

Kadhalika ameitaja sekta hiyo kama mbinu mojawapo ya kukuza uchumi wa kaunti hiyo sawia na ukosefu wa ajira miongoni mwa wakaazi wa kaunti ya Taita Taveta.

Total Views: 136 ,