Malindi ni mashindano kati yangu na Rais Uhuru,Asema Raila

RAILA NA UHURUKinara wa ODM Raila Odinga amesema uchaguzi mdogo wa ubunge katika eneo la Malindi kaunti ya Kilifi ni mashindano baina yake na rais Uhuru Kenyatta huku akiwarai wafuasi wa Cord kumchagua Willy Mtengo ili kudhihirisha kwamba eneo hilo ni ngome ya ODM.

Raila ambaye amepiga kambi katika eneo hilo kumpigia debe mgombea wa kiti hicho kwa tiketi ya chama cha ODM alizungumza katika uwanja wa Kwachocha ambako aliwarai wakaazi kupiga kura kwa uangalifu na kuepuka kile anachodai kuwa ahadi zisizotimia.

Raila anadai kuwa serikali imepoteza muelekeo kwa kujihusisha na ufisadi kutoka kashfa ya idara ya NYS hadi ile ya hati ya dhamana ya yuro na nyingine nyingi zitakazochipuka akisema pesa za mlipa ushuru hazitaendelea kupotea mikononi mwa viongozi wafisadi.

Mwisho

Total Views: 445 ,