Mali ya wizi iliyofichwa Uswizi kurejeshwa nchini asema Rais Uhuru

Kenya imetia sahihi mkataba wa maelewano kuhusu usaidizi wa kisheria na nchi ya Uswizi ili kufanikisha kurejeshwa kwa mali ya umma iliyopatikana kupitia njia ya ufisadi na uhalifu iliyofichwa nchini humo.

Akizungumza baada ya kutia sahihi mkataba huo rais wa uswizi Alain Berset aliye humu nchini,amesema kuwa mkataba huo unapania kuboresha zaidi mkataba wa maelewano uliopo kuhusu kurejeshwa kwa mali ya wizi akitoa mfano wa sakata ya Anglo Leasing.

Aidha mwenyeji wake rais Uhuru Kenyatta amempongeza kiongozi huyo wa uswizi akisisitiza kuwa mkataba huo ni wa manufaa katika makabiliano dhidi ya ufisadi yanayoendeshwa na serikali yake humu nchini.

Kadhalka ni katika mkutano huo ambapo rais Uhuru ametangaza mpango wa Kenya kufungua ubalozi wake nchini Uswizi kufikia mwezi wa kumi mwaka huu hatua inayolenga kuboresha uhusiano wa kidiplomasia baina ya nchi hizi mbili.

Mwisho

Total Views: 154 ,