Mali ya mamilioni yateketea katika shule ya upili ya mseto ya Mokowe kaunti ya Lamu

Mali ya thamani ya zaidi ya shillingi million 7.5 imeteketea katika shule ya sekondary ya mseto ya Mokowe huko Lamu magharibi huku visa vya moto vikikumba shule kadha wa kadha nchini.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo,Thaddeus Mugute ambaye alithibitisha kisa hicho amesema bweni moja la wanafunzi 93 liliteketea wakati wanafunzi walipokuwa kwenye masomo ya usiku.

Alisema takriban godoro 90,sare za shule na masanduku yaliharibiwa kwenye moto huo.

Uchunguzi unaendelea kubainisha chanzo cha moto huo.

Kisa hicho kimetokea huku serikali ikipendekeza kuwalazimu walimu kulipia gharama ya mali inayoharibiwa na wanafunzi shuleni.

Mwisho

Total Views: 144 ,