Makataa ya waasi wa chama yaisha leo

 

Makataa ya siku saba yaliyotolewa na kiongozi wa ODM Raila Odinga kwa magavana na wabunge 12 waliohama chama hicho na kujiunga na Jubilee yanakamilika leo.

Haya yana jiri huku chama hicho kikiwafahaisha wabunge wawili zaidi kuhusu mipango ya kutaka kuwafurusha chamani  kwa kujihusisha na vyama vingine pinzani.

Mbunge wa Likoni Masoud Mwahima na mwenzake wa Abudalang’i Ababu Namwamba aliyejiuzulu kama katibu mkuu wa ODM ndio wa hivi punde kulengwa na vitisho vya kufurushwa kutoka chamani.

Kadhalika imebainika kuwa magavana walioathirika,manaibu wao na wabunge wamekaidi agizo la chama hicho la kuwataka waelezee kwa nini hatua za kinidhamu zisichukuliwe dhidi yao kwa kujiunga na chama cha Jubilee na baadhi yao kuhudhuria hafla ya wazi iliyoongozwa na rais Uhuru Kenyatta.

Kulingana na mwenyekiti wa kamati ya nidhamu katika chama hicho Fred Athuko,kamati hiyo itakutana kupitia majibu kutoka kwa wanasiasa ikiwa yako na kusikiliza utetezi wao kabla ya kutoa mapendekezo kwa kamati kuu ya kitaifa ya ODM.

Total Views: 349 ,