MAKATAA KWA SERIKALI YA KAUNTI YA KWALE

Wahudumu wa afya katika kaunti ya Kwale wametishia kuandaa mgomo iwapo serikali ya kaunti hiyo haitatekeleza makubaliano baina yao kufikia tarehe 11 mwezi February mwaka huu.

Kwenye mazungumzo yanayoendelea baina ya  chama cha wahudumu  hao  na serikali ya kaunti  hiyo, wahudumu  wanataka nyongeza ya marupurupu  kutoka  elfu 20 hadi   elfu 30,nyongeza ya marupurupu ya sare za kazi kutoka elfu 10 hadi  elfu 25 na kupandishwa vyeo.

Wahudumu hao wanadai kuwa wamechoshwa na ahadi zizisoteketelezwa licha ya serikali ya kaunti hiyo kuahidi kulivalia njuga swala hilo.

Total Views: 66 ,