MAKANISA KUWAKATAZA WANASIASA IBADA

 

Makanisa ya kievanjilisti nchini yamesema kuwa yatawazuiya wanasiasa wanaowachechea wananchi dhidi ya kuhudhuria ibada katika makanisa hayo.

Kadhalika yamewataka wanaoeneza chuki nchini kuungama dhambi zao kabila ya uchaguzi mkuu mwaka ujao sawa na kuwahimiza wakenya kutowapigia kura.

Wakiongea katika kanisa la House Of prais kaunti ya Meru ,wakiongozwa na askofu mkuu wa makanisa hayo Mark Kariuki wamewakashifu wanasiasa wanaolenga makanisa na kuyatumia kujinufaisha kibinafsi.

Amesema kanisa litawachunguza kwa makini na kuwataja viongozi wote wanaochechea vurugu nchi inapoelekea kwenye uchaguzi   huo mkuu.

Askofu Kariuki alikuwa pamoja na makasisi na maaskofu wengine kutoka  kaunti hiyo ya Meru,Tharaka-Nithi na Isiolo.

Total Views: 332 ,