Makala ya Raga kuanza Nakuru

Malaka ya mwaka 2016 ya mchezo wa raga ya kitaifa kwa wachezaji saba kila upande yataanza mnamo tarehe 6 mwezi Agosti ,michezo ambayo itakuwa inatayarisha vilabu kushiriki kwa makala michezo ya safari sevens yatakayofanyika juma la mwiso la mwezi septemba.
Baada ya makala hayo ya nakuru itafatia makala ya Kabeberi jijini Nairobi, Driftwood Mombasa Sevens, Dala sevens huko Kisumu , Nanyuki na kisha kukamilisha na makala ya Christie sevens kabla ya safari sevens.
Top Fry Nakuru ndio mabingwa watetezi wa makala ya mwaka jana ambapo walimaliza katika nafasi ya kwanza wakiwa na alama 91.
1. Top Fry Nakuru 91pts
2. Mwamba 81pts
3. Kenya Harlequin 75pts
4. Pan Africa Strathmore Leos 73pts
5. Resolution Impala Saracens 69pts
6. Menengai Cream Homeboyz 67pts
7. KCB 67pts
8. Kabras Sugar 56pts
9. Total Nondies 41 pts
10. Western Bulls 38pts

Total Views: 318 ,