Makabiliano ya KipinduPindu Mombasa

Idara ya afya katika kaunti ya Mombasa imezindua vituo vya kutibu maradhi ya kipindupindu ili kukabiliana na chamuko la hivi punde la ugonjwa huo ambalo tayari limesababisha vifo vya watu wawili.

Waziri wa afya katika serikali ya kaunti ya Mombasa, Hazel Koitaba, amesema vituo vya afya vitatumika kama vituo vya kutibu ugonjwa huo ambao umeenea hadi mitaa ya mabanda.

Amedokeza kuwa jumla ya wagonjwa 25 wanaougua maradhi ya kipindupindu wametengwa ambapo wamelazwa katika kituo cha afya cha Mwembe Tayari huku akiutaka umma kutafuta matibabu mara moja iwapo watahisi dalili za maradhi hayo.

Kaunti ya Mombasa imekuwa ikijizatiti kukabiliana na ugonjwa wa kipindupindu ambao ulizuka wiki mbili zilizopita ambapo kwa mujibu wa Koitaba mkurupuko huo unatokana na vidimbwi vya maji ya mvua iliyoshuhudiwa ambavyo kwa sasa vinapulizwa dawa.

Mwisho

Total Views: 262 ,