Makabiliano dhidi ya Fistula Kilifi

Waziri wa afya katika kaunti ya Kilifi Rachael Musyoki ametoa wito wa kutolewa kwa uhamasisho zaidi kwa umma kuhusiana na ugonjwa wa fistula kwa manufaa ya wakaazi wa kaunti hiyo na nchi yote kwa jumla.

Haya yamejiri huku Kenya ikijiunga na ulimwengu kuadhinisha mwezi wa ugonjwa wa fistula.

Musyoki alisema hata hivyo Kenya itaendeleza kampeni dhidi ya ugonjwa huo hata baada ya kukamilika kwa muda wa mwezi huo mmoja ili kuhakikisha wagonjwa wengi zaidi wanahudumiwa kwenye harakati ua kuwanasua kutoka kwa matatizo hayo.

Musyoki alisema haya huku wanawake 20 kutoka kaunti ya Kilifi wakinufaika na matibabu ya ugonjwa wa fistula bila malipo huduma zilizofadhiliwa na serikali ya kaunti ya Kilifi kwa ushirikiano na mashirika ya AMREF na wakfu wa Freedom from Fistula.

Mwisho

Total Views: 384 ,